Rais aonya dhidi ya udhalilishaji wa wanawake wanaposaka ajira

  • | K24 Video
    34 views

    Rais William Ruto ameonya vikali dhidi ya udhalilishaji wa wanawake wanaotafuta ajira katika mradi wa ujenzi nyumba za bei nafuu. Rais ambaye amezungumza baada ya kuzindua mradi huo eneo bunge la Starehe jijini Nairobi, amesema wenyeji watapewa kipaumbele katika umiliki wa nyumba hizo zitakazojengwa na mbunge wa eala suileman shabal wa muungano wa Azimio kupitia kampuni yake ya Gulf capital. Kwa upande wake naibu rais Rigathi Gachagua amewakaribisha wabunge wa Azimio kuungana na serikali kwa madhumuni ya ajenda ya maendeleo. Mbunge wa Langata Felix Oduor almaarufu jalango na mbunge wa Dagoretti kaskazini Beatrice Elachi kutoka muungano wa Azimio ni miongoni mwa wabunge waliohudhuria