Rais Biden na Rais wa China wakubaliana kuanzisha tena mazungumzo ya kijeshi

  • | VOA Swahili
    389 views
    Rais wa Marekani Joe Biden alikutana na Rais wa China Xi Jinping siku ya Jumatano nje ya San Francisco, ambako viongozi wa uchumi wa Asia-Pacific wanakusanyika. Biden - ambaye alisema bado anamwona kiongozi wa china kama "dikteta" - alisema wawili hao walikubali kuanzisha tena mazungumzo ya kijeshi, kufanya kazi pamoja kutathmini vitisho vinavyoletwa na ujasusi bandia, na kuchukua hatua za maana ili kukabiliana na suala la dawa ya fentanyl. #VOASwahili Sauti ya Amerika - Idhaa ya Kiswahili inawafikia zaidi ya watu milioni 100 wanaotembelea tovuti, mitandao ya kijamii, radio na televisheni zetu. Tunawasilisha maudhui kuhusu Afrika Mashariki na Kati kwa nchi takriban 11 huko Afrika na wale walioko ughaibuni na kwingineko duniani. Vipindi vyetu vimejikita katika maudhui mbalimbali ikiwemo habari, vijana, wanawake, siasa, sayansi, teknolojia, afya, biashara, michezo, muziki na burudani na pia tunawashirikisha wasikilizaji wetu.