MUSTAKABALI WA JUBILEE
Rais mstaafu Uhuru Kenyatta ameonya kwamba ufanisi ulioafikiwa chini ya utawala wake uko kwenye hatari ya kubatilishwa na serikali ya Kenya Kwanza. Akirejelea wasiwasi wa umma kuhusiana na utekelezaji wa halmashauri ya afya ya jamii-SHA, Kenyatta alitahadharisha dhidi ya kufanya majaribio na miradi ya serikali badala ya kuangazia maslahi ya umma. Rais huyo mstaafu aliyasema hayo katika mkutano wa kitaifa wa wajumbe wa chama cha Jubilee, ulioafiki kufanyia marekebisho katiba yake, hatua ambayo imechukuliwa kuwa fursa mwafaka ya kumteua aliyekuwa waziri wa usalama Fred Matiang’i kuchukua mahala pa Kenyatta kuwa kinara wa chama hicho.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive