Rais Ruto aahidi kuwa serikali imejizatiti kuangazia maslahi ya kijamii

  • | Citizen TV
    1,759 views

    Serikali imetenga shilingi bilioni 28 kutoa msaada kwa wasiojiweza kwenye jamii ili kuwainua kiuchumi. Rais william ruto amesema kuwa serikali na jamii kwa jumla ina jukumu la kuwainua wasiojiweza na kuimarisha hali yao ya kimaisha. Alizungumza kwenye kongamano la kuangazia maslahi ya kijamii hapa jijini Nairobi, ambako washika dau na washirika wa kimaendeleo wanakongamana. Baadaye leo, rais ruto anatarajiwa kusafiri hadi rwanda kwa ziara rasmi ya siku mbili.