Rais Ruto afutilia mbali bili ya hospitali ya Mukami Kimathi, mkewe Dedan Kimathi

  • | KBC Video
    463 views

    Rais William Ruto amefutilia mbali bili ya hospitali ya Mukami Kimathi, mkewe mpiganiaji wa uhuru wa Kenya Dedan Kimathi. Mukami alikuwa amezuiliwa katika hospitali moja jijini Nairobi baada ya familia yake kushindwa kulipa zaidi ya shilingi milioni 1.3 za bili za hospitali. Naibu Rais Rigathi Gachagua aliyemtembelea Mukami Kimathi katika hospitali hiyo, alisema kuwa serikali ya Kenya Kwanza inaangazia masaibu ya wapiganiaji uhuru, ambao bado wako hai na wanakabiliwa na umaskini licha ya kupigania uhuru wa nchi hii.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.com/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1news Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #KBCchannel1 #KenyaElection2022 #News