Rais Ruto akiri kukutana na kinara wa upinzani

  • | Citizen TV
    9,793 views

    Rais William Ruto amekiri kuwa alikutana na kinara wa upinzani Raila Odinga na kutoa masharti ya jinsi mazungumzo yataendeshwa. Akizungumza katika ibada ya shukrani kaunti ya Kwale, rais alisema suala la ongezeko la gharama ya maisha haitatatuliwa kupitia mazungumzo ila kwa mipango ya serikali aliyosema ipo ndani ya manifesto ya Kenya Kwanza.