Rais Ruto asema serikali itasimama kidete kuwalinda polisi

  • | Citizen TV
    11,125 views

    Rais William Ruto amesema kuwa serikali itasimama kidete kuwalinda maafisa wa polisi wanapotekeleza wajibu wao wa kudumisha usalama wa taifa, hasa katika mazingira ya maandamano. Akizungumza katika kikao na wakuu wa usalama, Rais amesema serikali haitakubali maafisa wa polisi kuwa walengwa wa mashambulizi kutoka kwa raia. Aidha Waziri wa Usalama Kipchumba Murkomen amekana kutoa amri ya polisi kuwaua waandamanaji.