Rais Ruto ataka Afrika kufanisha maendeleo yake kwa kujikimu

  • | Citizen TV
    3,632 views

    Rais William Ruto ameutaka muungano wa bara Afrika kufanya hima na kujikimu kuhusu masuala ya maendeleo, uchumi na ustawishaji bila kutegemea misaada kutoka mataifa ya magharibi. Akizungumza katika mkutano wa tano wa muungano huo Rais William Ruto pia alipendekeza kuwe na mabadiliko kwani ilivyo sasa asilimia sitini ya miradi ya au inafadhiliwa na wafadhili wa nje. Kati ya marais waliokuwemo kwenye mkutano huo katika makao makuu ya Umoja wa Mataifa ya UNDP eneo la Gigiri, ni pamoja na Azali Assoumani wa Comoros, Ali Bongo wa Gabon, Abdel Fattah wa Misri, Macky Sall wa Senegal, Ismail Guelleh wa Djibouti, Bola Tinubu wa Nigeria na mwenyekiti wa Muungano wa Bara Afrika Moussa Faki.