- 1,051 viewsDuration: 2:46Wakazi wa Kisumu sasa wameelezea matumaini yao ya kuimarika kwa hadhi ya maisha kufuatia uzinduzi wa awamu ya pili ya ujenzi wa reli ya SGR. Kando na kutoa nafasi za ajira, wakazi hao pia wanaitaka serikali kuharakisha ulipaji wa fidia kwa wale watakaohamishwa wakati wa ujenzi wa reli hiyo. Rais William Ruto anatarajiwa kuzindua ujenzi wa reli hiyo Jumamosi katika hafla itakayohudhuriwa na watu zaidi ya elfu ishirini