Rais Ruto kulihutubia taifa kutoka bungeni hapo kesho

  • | K24 Video
    75 views

    Rais William Ruto ametakiwa kuelezea mustakabali wa mazungumzo ya kitaifa yanayoendelea baina ya serikali na upinzani wakati wa hotuba yake ya kwanza kwa taifa bungeni hapo kesho. Rais pia anakabiliwa na matarajio ya wakenya kuhusu afueni ya kiuchumi ambapo wengi wanasema hawawezi kumudu tena gharama ya maisha ya sasa.Rais anatarajiwa kuelezea mafanikio ya serikali ya Kenya Kwanza ambayo iko katika mwaka wake wa pili tangu iingie madarakani.