Rais Ruto kuzindua kampeini za Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika

  • | Citizen TV
    1,914 views

    Marais kadhaa wa Afrika Mashariki wanatarajiwa nchini hapo kesho, wakati Rais William Ruto atakapoongoza uzinduzi wa safari ya Raila Odinga kuwania uwenyekiti wa Tume ya Umoja wa Afrika. Serikali sasa ikisema kuwa, kampeni ya kumpigia debe raila itaanza pindi baada ya uzinduzi wa kesho.