Rais Ruto na Raila wakosoa uamuzi wa mahakama kuhusu usajili wa makundi ya mashoga na wasagaji

  • | K24 Video
    89 views

    Katika hafla tofauti, Rais William Ruto na kiongozi wa upinzani Raila Odinga wamekuwa na msimamo mmoja. msimamo wa kupinga vikali na kukashifu uamuzi wa mahakama ya juu wa kuruhusu usajili wa makundi ya mashoga na wasagaji. Rais anasema ingawa anaheshimu mahakama hawezi kuruhusu ndoa za jinsia moja. Raila naye amieshutumu mahakama kwa kujipa mamlaka yasiyokuwa yake kwa kuunda sheria ambayo ni mamlaka ya bunge.