Simba wa kufugwa atoroka na kushambulia mama na watoto mtaani

  • | BBC Swahili
    3,111 views
    Polisi nchini Pakistani wamewakamata wamiliki wa simba aliyemshambulia mwanamke mmoja na watoto wake. Picha za CCTV kutoka jiji la mashariki la Lahore zilionyesha jinsi simba huyo mkubwa alivyotoroka kwa kuruka ukuta na kumfukuza mwanamke huyo huku mashuhuda waliojawa na hofu wakikimbia kwa usalama wao. Mwanamke huyo na watoto wake, wenye umri wa miaka mitano na saba, walipata majeraha kwenye mikono na nyuso zao lakini sasa wako katika hali nzuri. #bbcswahili #pakistan #wanyama Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw