Rais wa Tanzania Samia Suluhu asema anatetea amani ya nchi yake

  • | Citizen TV
    13,502 views

    Serikali ya marekani sasa inataka uchunguzi kufanywa na wahusika wa mateso ya wanaharakati wa kenya na uganda nchini tanzania kutiwa mbaroni. mkenya boniface mwangi na agather atuhaire wa uganda walikamatwa na kuteswa na maafisa wa usalama nchini tanzania kwa madai ya kumuunga mkono kiongozi wa upinzani nchini humo Tundu Lissu. hata hivyo, rais wa tanzania samia suluhu amesema kuwa ataendelea kuilinda nchi yake dhidi ya kuingiliwa na wageni.