Rais William Ruto ametangaza kusitishwa kwa uajiri wa walimu elfu ishirini

  • | K24 Video
    32 views

    Rais William Ruto ametangaza kusitishwa kwa uajiri wa walimu elfu 20 kufuatia nakisi ya bajeti iliyotokana na kufutiliwa mbali kwa mswada wa fedha wa 2024. hatahivyo ameahidi walimu watarajali wa jss elfu 46 kuwa bado wataajiriwa kupitia ufadhili wa shilingi bilioni 18.3. wakati huohuo, chama cha walimu wa shule za upili ,kuppet, kimeshtumu kuondolewa kwa bajeti ya kutahini ya shilingi bilioni 5, huku kikihofia kuwa baraza la mitihani ya kitaifa (KNEC) huenda likakosa kutahini wanafunzi au ikalazimu wazazi kugharamia ada hiyo. ili kupunguza bajeti, KUPPET imeshauri serikali kukata bajeti ya shilingi bilioni 12 ya ujenzi wa madarasa zaidi ya elfu 15 na badala yake kuruhusu wanafunzi wa gredi ya 9 kuhamia katika shule za sekondari