Rais William Ruto anaongoza kikao cha maafisa wakuu serikalini kutathmini utendakazi wao

  • | Citizen TV
    660 views

    Rais William Ruto anaongoza kikao cha maafisa wakuu serikalini katika eneo la South C hapa jijini. Kikao hicho kinawajumuisha naibu rais, mawaziri, makatibu, baraza la washauri na linalenga kutathmini mwaka mmoja wa serikali ya Kenya Kwanza. Haya yanajiri wakati ambapo wakenya, viongozi wa upinzani pamoja na viongozi wa dini wamelalamikia gharama ya juu ya maisha na kuitaka serikali kuangazia tena mfumo wa ushuru ambao umeathiri pakubwa uchumi wa taifa