- 2,120 viewsDuration: 3:27Ripoti mpya iliyotolewa na Wakfu wa Kofi Annan imeonya kuwa kuna uwezekano mkubwa wa kutokea kwa ghasia katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao. Ripoti hiyo kuhusu hatari ya machafuko ya uchaguzi imeangazia mtindo wa vurugu unaojitokeza kila Kenya inapokuwa katika kipindi cha uchaguzi. Kwa mujibu wa ripoti hiyo, kampeni za fujo, matokeo yanayopingwa mara kwa mara, ukabila na ukosefu wa imani kwa asasi za umma na serikali ni miongoni mwa sababu kuu zinazochochea ghasia za uchaguzi.