- 212 viewsDuration: 10:03Kampuni ya Royal Media Services imeandaa msururu wa shamrashamra za kuadhimisha miaka 10 ya utangazaji bora wa Inooro TV. Sherehe hizi zimepangwa kuwaleta pamoja watangazaji wa Inooro TV na mashabiki wao katika maeneo mbalimbali ya eneo la Kati.Tangu kuzinduliwa mwaka 2015, Inooro TV imesalia kileleni katika utangazaji kwa lugha ya Kikuyu ishara ya ukakamavu wa Royal Media Services katika kuwapa watazamaji wake habari tendeti, burudani, na vipindi vya kuelimisha.