Skip to main content
Skip to main content

Ruto akabidhi Migori Youth FC basi jipyaScript:

  • | Citizen TV
    672 views
    Duration: 1:40
    Rais William Ruto ameikaribisha Migori Youth FC, mabingwa wa Ligi ya Taifa (NSL), katika Ikulu ya Nairobi ambako timu hiyo iliwasilisha kombe lake na kupokea basi jipya aliloiahidi. Wakiongozwa na mwenyekiti wao, Aziz Abdi Osman, viongozi wa timu hiyo walimshukuru Rais na kumwomba aendelee kuiunga mkono wanapoanza safari ya kucheza Ligi Kuu kwa mara ya kwanza baada ya miaka 20. Rais Ruto alikabidhi basi hilo akisema litasaidia kurahisisha usafiri wa timu hiyo katika mechi za kitaifa. Mapema akiwa Kaunti ya Migori, Rais alisema serikali inaendelea kujenga uwanja wa kisasa ili kutoa mazingira bora ya kukuza vipaji vya vijana na kuimarisha maendeleo ya soka nchini.