- 390 viewsRais William Ruto sasa anaitaka nchi za Afrika na washirika wake wa kimataifa kuchangia katika kikapu cha fedha kitakachosaidia kuhakikisha kuwa maeneo yaliyo kando ya Mto Congo Basin hayabaki nyuma katika ufadhili wa kukabiliana na changamoto za mabadiliko ya tabianchi. Akizungumza katika mkutano wa marais na viongozi wa serikali uliofanyika katika State House Nairobi, Ruto aliwaomba wawekezaji wa kimataifa kutambua thamani kamili ya rasilmali za mataifa ya Afrika na kuwekeza zaidi katika miradi ya mazingira na maendeleo endelevu.