Sakaja asema Nairobi itaimarika kwa ulipaji wa kodi zaidi

  • | Citizen TV
    1,309 views

    Gavana wa kaunti ya Nairobi Johnson Sakaja ametetea mapendekezo ya kuongeza ada na kodi mpya za kufanyia biashara katika kaunti ya Nairobi. Sakaja amesema mapedekezo hayo bado yatajadiliwa na wananchi kabla ya kuidhinishwa kuwa sheria. Gavana Sakaja pia amesema kuwa kaunti ya Nairobi inakamilisha mfumo wa kidijitali utakaowezesha wafanyibiashara na wakaazi wa nairobi kulipa kodi na ada zozote kwa njia ya kidijitali na kuondoa ufisadi.