Seneta Khalwale apinga vikali ubinafsishaji wa viwanda vya sukari katika eneo hilo.

  • | K24 Video
    132 views

    Kiranja wa wengi katika bunge la Seneti Dkt Bonnie Khalwale ameongoza viongozi wa eneo la Magharibi kupinga vikali ubinafsishaji wa viwanda vya sukari katika eneo hilo. Seneta huyo wa Kakamega amesema japo ni kiongozi katika serikali ya Kenya Kwanza, hilo halitamzuia kutetea haki za wenyeji wa Magharibi. Ni hoja iliyoungwa mkono na viongozi wa mrengo wa Azimio katika hafla tofauti ambao wametoa changamoto kwa spika wa bunge la kitaifa Moses Wetangula kuhakikisha hilo halitimii chini ya uongozi wake.