Skip to main content
Skip to main content

Seneta Nyamu aomba msamaha bungeni kufuatia kauli zake

  • | Citizen TV
    3,144 views
    Duration: 1:53
    Seneta Maalum wa chama cha UDA Karen Nyamu alilazimika kuomba msamaha bunge la Seneti kuhusu matamshi aliyotoa.Katika kitendo cha kushangaza na cha aibu, Nyamu mnamo mwezi machi alitoa matamshi ya kumdhalilisha mwanafunzi wa Gredi ya 10 aliyekuwa amefika Seneti kwa mafunzo maalum. Matamshi hayo yaliibua hisia kali huku spika wa muda Veronica Maina akimtaka Nyamu aombe msamaha mara moja. Hata hivyo msamaha aliotoa Nyamu pia umekosolewa huku aliyekuwa Rais wa chama cha mawakili LSK, Faith Odhiambo akilitaka bunge la Seneti kuchukua hatua zaidi dhidi ya Seneta huyo..