Serikali imegharamia matibabu ya shilingi bilioni 6.8 kupitia SHA

  • | KBC Video
    28 views

    Wakenya milioni 24.8 wamesajiliwa kwa halmashauri ya afya ya jamii SHA, huku wagonjwa milioni 4.5 wakipokea matibabu ya magonjwa ya kawaida na huduma za uzazi, kupitia hazina ya huduma za msingi tangu ilipozinduliwa mnamo Oktoba mosi mwaka wa 2024. Chini ya hazina ya afya ya jamii, wakenya milioni 2.2 wamenufaika kutokana na huduma maalum, zaidi ya wagonjwa elfu 800 wanapokea matibabu ya figo, elfu 18 wanatibiwa saratani, huku visa elfu 550 vya kujifungua vikishughulikiwa.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive