Serikali imetangaza kupunguza bei ya gesi na maziwa

  • | K24 Video
    234 views

    Naibu rais Rigathi Gachagua amesema serikali ya William Ruto inalenga kupunguza bei ya bidhaa muhimu kama vile gesi na wala sio kusambaratisha biashara za baadhi ya wafanyibiashara waliopo katika upinzani. Gachagua amesema haya katika hafla ya ibada ya kanisa la Jesus Winners Ministries Roysambu jijini Nairobi. Akiandamana na gavana Johnson Sakaja pia ametangaza kuwa hawana tofauti kama inavyodaiwa na baadhi ya wapinzani wao.