Serikali inalenga kupanda miche milioni 6 Kaunti la Migori

  • | Citizen TV
    230 views

    Serikali kupitia wizara ya elimu inalenga kupanda miche milioni 6 katika Kaunti ya Migori kabla ya mwisho wa Juni 2024 katika zoezi linaloendelea la upanzi wa miti kote nchini. Takwimu kutoka wizara ya elimu zinaonyesha kuwa miche milioni 2 imepandwa katika shule za kaunti ya Migori katika muda wa mwezi mmoja uliopita. Mkurugenzi wa elimu kanda ya Nyanza Nelson Sifuna alisema kila mwanafunzi atapanda angalau miti minne na kila mwalimu atapanda miti kumi katika shule zao. Alikuwa akizungumza wakati wa uzinduzi wa zoezi la upandaji miti katika shule ya upili ya wasichana ya Ulanda katika kaunti ndogo ya Awendo