- 912 viewsDuration: 3:13Hazina ya Taifa imetangaza mipango ya serikali ya kuuza asilimia 15 ya hisa zake katika kampuni ya huduma za mawasiliano ya simu ya Safaricom. Kulingana na serikali, hatua hiyo itaisaidia kupata shilingi bilioni 244.5 zitokozwa katika hisa zaidi ya milioni 6 zitakazohamishwa kwa kampuni ya vodafone Kenya. Hata hivyo, Wizara ya Fedha inasisitiza kuwa Kampuni hiyo itabaki kuwa chapa ya Kenya, ikiorodhesha masharti kadhaa ambayo yanapaswa kutimizwa kama sehemu ya makubaliano ya uuzaji wa hisa hizo