Serikali ya kaunti ya Taita Taveta yatenga Shilingi milioni 50 kukuza na kuongeza thamani ya mpunga

  • | Citizen TV
    125 views

    Serikali ya kaunti ya Taita Taveta imetenga Shilingi milioni 50 ili kukuza na kuongeza thamani ya mpunga katika kaunti hio. Gavana Andrew Mwadime amezindua rasmi mradi wa mambomba ya kunyunyizia maji mashamba ya mpunga ili kuwafaidi zaidi ya wakulima 300 eneo hilo. Aidha kaunti hiyo inapania kukuza mtama katika ekari 30,000.