Serikali yapiga marufuku shughuli za baharini eneo la pwani

  • | Citizen TV
    1,203 views

    Serikali imepiga marufuku shughuli za uvuvi, kuogelea na utalii kwenye fuo za bahari ili kukabiliana na hatari ya mawimbi makali yanayotarajiwa katika kipindi cha siku tatu zijazo. Kamanda wa polisi pwani, ali nuno amedokeza kwamba hatua hiyo ni ya kudhibiti uwezekano wa maafa kutokana na mawimbi hayo yanayoendelea kushuhudiwa. Upepo mkali tayari umeanza kushuhudiwa kaunti ya mombasa huku maafisa wa polisi wakionya kuwa atakaye vunja sheria hiyo atachukuliwa hatua.