- 187 viewsDuration: 1:18Serikali inalenga kupanua mradi wa Galana Kulalu ili kuimarisha utoshelevu wa chakula sambamba na kukabili baa la njaa linalokumba zaidi ya kaunti 20 kote nchini. Akizungumza alipozuru mradi huo, waziri wa Maji na unyunyizi Eric Mugaa amesema serikali iko mbioni kuongeza ekari 10,000 kwa mradi huo ili kufikisha kiwango cha ekari 20,000 zinazozalisha chakula.