Serikali yaweka mikakati kukomesha uhasama wa ardhi Angata Barikoi

  • | KBC Video
    73 views

    Rais William Ruto ameelezea kusikitishwa na makabiliano makali yaliyoshuhudiwa kati ya wakazi na polisi huko Angata Barikoi katika eneo la Narok akisema matukio sawia hayafai kutokea tena nchini. Akizungumza alipowasilisha hati za kumiliki ardhi kwa wakazi wa eneo la Emurua Dikir, Ruto alisema amekutana na wazee wa jamii za Wakalenjin na Wamaasai ambao waliafikiana kusuluhisha mzozo wa ardhi ya ekari elfu sita uliosababisha vifo vya watu watano na wengine kadhaa kujeruhiwa. Anavyotuarifu Abdiaziz Hashim Serikali itafidia au kutoa ardhi mbadala kwa familia zilizofurushwa kutoka Msitu wa Mau.

    Connect with KBC Online; Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKN Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1 Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV Check our website: https://www.kbc.co.ke/

    #kbcchannel1 #news #kbclive