- 110 viewsDuration: 1:24Serikali ya kenya imezindua mpango maalum ya utafiti na uokoaji ikiashiria maendeleo makubwa katika mfumo wa kukabiliana na majanga nchini . Mpango huu ni matokeo ya juhudi za ushirikiano kati ya Kitengo cha Kitaifa cha Usimamizi wa Maafa (NDMU) , kitengo cha Huduma kwa Polisi cha kukabiliana na majanga, vikosi vya zimamoto vya kaunti za Kiambu na Nairobi, pamoja na Kituo cha taifa la Poland cha Msaada wa Kimataifa (PCPM).