- 64 viewsWagonjwa wa saratani katika hospitali ya kitaifa ya Kenyatta wana hofu kuhusu uhaba wa dawa unaowalazimu kununua dawa za ghali kutoka maduka za kibinafsi nje ya hospitali. Licha ya kutumia bima ya afya ya SHA, wagonjwa hao wanasema gharama kubwa ya dawa hizo nje ya hospitali inamaliza kwa haraka bima yao ya matibabu, na kusababisha washindwe kukamilisha matibabu yao.