7,312 views
Duration: 47s
Idadi ya watu waliouawa katika shambulizi la risasi mjini Jerusalem imeongezeka hadi sita, kwa mujibu wa waziri wa mambo ya nje wa Israel Gideon Saar.
Tukio hilo limetokea kwenye kituo cha basi mjini Jerusalem siku ya Jumatatu, huku polisi wakisema wahalifu hao wameuawa.
Haikufahamika mara moja ni nani aliyetekeleza shambulio hilo. Lakini kundi la wanamgambo la Hamas limewasifu "wapiganaji" wawili wa Kipalestina ambao limesema wamefanya shambulio hilo, ila Hamas haijadai kuhusika.
Kwa mengi zaidi, jiunge na @elizabethkazibure katika dira ya dunia TV saa tatu kamili, pamoja na mtandao wa YouTube wa BBC Swahili ambapo tunapatikana mubashara.
#bbcswahili #Jerusalem #israel
Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw