Shirika la Red Cross lalazimika kutumia boti za uokoaji kuokoa mafamilia katika eneo la Madogo

  • | Citizen TV
    1,721 views

    Huku mafuriko yanapoendelea kuhangaisha wakaazi wa maeneo mengi nchini, hali maeneo ya Kaskazini Mashariki imeendelea kusababisha athari za kipekee. Katika eneo la Madogo lililo kwenye mpaka wa kaunti za Tana River na Garissa, hali imesalia kuwatatiza wengi kwani barabara inayounganisha kaunti hizi mbili haipitiki. Kwa sasa, maafisa wa shirika la Red Cross wamelazimika kutumia boti za uokoaji.