Shughuli za uvunaji miti zimeshika kasi misituni baada ya rais kuondoa marufuku

  • | Citizen TV
    3,245 views

    Mwezi mmoja baada ya Rais William Ruto kuondoa marufuku ya uvunaji wa miti kwenye misitu nchini, shughuli hiyo imeanza kwa kasi huku waliopewa leseni ya kukata miti kabla ya marufuku kuwekwa mwaka wa 2018 wakiruhusiwa ndani ya misitu. Idara ya misitu imewapa kibali cha kukamilisha uvunaji huku utaratibu wa kutoa leseni kwa watu zaidi kukata miti katika hekta 5,000 iliyo na miti iliyokoma ikiendelea. Japo wafanyibiashara wameshabikia hatua hiyo, wanamazingira wanahofia huenda juhudi za kulinda misitu zikaathirika. Gatete Njoroge alizuru misitu mbalimbali ambako uvunaji wa miti unaendelea na kuandaa makala haya.