Skip to main content
Skip to main content

Shule kadhaa Laikipia zafungwa kutokana na uvamizi wa majambazi

  • | Citizen TV
    1,212 views
    Duration: 5:08
    Shule kadhaa katika eneo la Laikipia Kaskazini zimefungwa kutokana na kuongezeka kwa hali ya ukosefu wa usalama, hali iliyoacha mamia ya wanafunzi bila masomo na kuwalazimu kuungana na wazazi wao kujificha katika shule zilizogeuzwa kuwa makazi ya muda wakitafuta usalama. Mashambulizi ya majangili yaliyotokea kwa siku nne mfululizo yamesababisha watu wawili kujeruhiwa na kuibiwa kwa zaidi ya mifugo 1,500. Mashambulizi haya ya mara kwa mara yamesababisha wakazi kuhama kwa wingi, wakikimbia makazi yao kutafuta usalama.