Shule zafunguliwa, licha ya mvua kuharibu miundomsingi

  • | Citizen TV
    1,988 views

    Ni rasmi sasa, muhula wa pili kwa wanafunzi wa shule za msingi na sekondari utaanza Jumatatu baada ya kucheleweshwa kwa wiki mbili. Rais William Ruto ametangaza kufunguliwa kwa shule baada ya utabiri wa hali ya anga kueleza kuwa mvua kubwa ambayo ilisababisha kuahirishwa kwa masomo itapungua katika siku zijazo. Tangazo ambalo ni afueni kwa baadhi ya wazazi na wanafunzi lakini ni kero kwa wale ambao miundo misingi ya shule zao iliathiriwa na mafuriko.