Tume ya utekelezaji haki imeeleza wasiwasi kuhusu ukosefu wa uwazi katika utoaji taarifa za mashirika ya serikali, hali inayowafanya wananchi washindwe kuwawajibisha viongozi. Tume hiyo inasema ipo haja ya kuwaelimisha wananchi kuhusu mbinu zilizopo za kupata taarifa hizo. Katibu katika wizara ya habari, mawasiliano na teknolojia Mhandisi John Tanui, amesema serikali imeweka huduma 22,000 mtandaoni ili kurahisisha upatikanaji wa taarifa na kupunguza pengo la mawasiliano.
Connect with KBC Online;
Subscribe to our channel: https://t.ly/86BKNc
Follow us on Twitter: https://twitter.om/KBCChannel1
Find us on Facebook: https://www.facebook.com/kbcchannel1TV
Check our website: https://www.kbc.co.ke/
#kbcchannel1 #news #kbclive