Siku ya Vitiligo yaadhimishwa kwa kutoa hamasisho

  • | Citizen TV
    192 views

    Chama cha vitiligo nchini Kenya kimeadhimisha siku ya vitiligo duniani jijini Nairobi kwa lengo la kuhamasisha watu kuhusu ugonjwa wa vitiligo unaosababisha kupotea kwa rangi ya ngozi na mabaka mepesi kwenye ngozi. Siku hii iliadhimishwa kwa matembezi kuzunguka Nairobi CBD na huduma za uchunguzi wa matibabu bila malipo, dawa za vipodozi na matibabu ya kisaikolojia zinazolenga kuongeza ufahamu kuhusu ugonjwa wa ngozi. Sherehe za mwaka huu zililenga uhamasishaji na uwezeshaji wa watu wanaoishi na vitiligo. Sherehe hizo ambazo zilipangwa kufanyika tarehe 25 ziliahirishwa kwa sababu ya maandamano.