Simu za wizi zanaswa Nairobi

  • | K24 Video
    183 views

    Maafisa wa polisi hapa Nairobi eneo la Industrial area wamewakamata washukiwa watano wakiwemo raia wa Burundi ambao walikuwa na simu za wizi walizokuwa wazisafirishe hadi nchini Burundi. Uchunguzi wa polisi umebaini kuna genge maalumu ambalo limepata soko ya simu za wizi katika nchi hiyo na pia kubaini simu nyingi ambazo huibiwa hapa nchini husafirishwa nje ya nchi na ndio maana huwa ni vigumu kuzipata.