Spika Wetangula aidhinisha hoja ya kumbandua Waziri Linturi

  • | Citizen TV
    1,081 views

    Spika wa bunge la taifa Moses Wetangula ameidhinisha hoja ambayo imewasilishwa bungeni ya kumtaka waziri wa kilimo Mithika Linturi kuondolewa mamlakani. Kulingana na hoja hiyo iliyowasilishwa na mbunge wa Bumula Jack Wamboka, waziri huyo anakabiliwa na tuhuma za utumizi mbaya wa mamlaka mbali na ukiukaji wa sheria. Akitoa uamuzi wake bungeni, spika Wetangula alisema kwamba ameridhishwa na malalamishi yalioyowasilishwa mbele yake na kutangaza mjadala kuhusu hoja hiyo itafanyika siku ya Alhamisi wiki hii.