Taharuki yatanda kaunti ya Garissa ambako koo mbili zaendeleza uhasama

  • | Citizen TV
    1,578 views

    Taharuki imeendelea kutanda kaunti ya Garissa ambako koo mbili zimeendeleza uhasama ambayo kufikia sasa umesababisha vifo vya watu sita. Ripoti za punde hata hivyo zinaarifu kuwa idadi ya waliouawa imeongezeka, saa chache baada ya waathiriwa wengine kuzikwa hapo jana. Mapigano hayo yameripotiwa katika eneo la Kunaso, na ripoti zaidi zinaarifu kuwa gavana wa Garissa Nathif Jama amelazimika kuondoka kutoka mkutano wa ugatuzi unaoendelea Eldoret kurejea Garissa.