Talanta na michezo kushirikishwa kuinua kiwango cha utalii kaunti ya Kwale

  • | Citizen TV
    73 views

    Wizara ya Huduma za Jamii na Talanta na ile ya Utalii katika kaunti ya Kwale zimesema talanta na michezo zinashirikishwa katika kuinua kiwango cha utalii katika kaunti hiyo. Wakizungumza katika hafla ya mbio za kila mwaka za Diani Run mawaziri wa idara hizo Francisca Kilonzo na Michael Mutua wamesema michezo tofauti inayoandaliwa eneo la Diani imeendelean kuuza eneo hilo kama kivutio kikuu mbali na kunoa talanta za vijana wa kaunti hiyo. Mbio hizo zilizoandaliwa na serikali ya kaunti ya Kwale kwa ushirikiano na South Coast Runners zimelenga kuhamasisha vijana kujitenga na visa vya utumizi wa dawa za kulevya na badala yake kuimarisha vipaji vyao katika nyanja tofauti. Lawrence Ng'ang'a anaarifu kutoka Kwale.