Skip to main content
Skip to main content

Tanzania imezindua mbinu mpya ya kusaidia kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK)

  • | BBC Swahili
    3,376 views
    Duration: 2:10
    Mbinu ya Teaching at the Right Level (TaRL) inaendeleakuwasaidia wanafunzi wenye changamoto za kusoma nakuandika kurejesha uwezo wao wa kujifunza. Miongonimwao ni Halima Hussein, mwanafunzi wa darasa la sita, ambaye awali hakuweza kusoma wala kuandika kwa ufasaha, lakini sasa anafanya vizuri darasani na ana matumaini yakufaulu mtihani wake wa kumaliza elimu ya msingi. Mafanikio hayo yanaakisiwa pia kwenye takwimu za hivi karibuni zinazoonyesha kuwa asilimia 79 ya wanafunzi wanauwezo wa kusoma na asilimia 70 wanamudu kuandika, mafanikio yanayohusishwa na matumizi ya mbinu mbalimbaliza ufundishaji. Katika kuimarisha juhudi hizo, Tanzania imezindua Mpango Mkakati wa Kisayansi wa Kujenga Umahiri wa kusoma,kuandika na kuhesabu (KKK). Mwandishi wa BBC, Humphrey Mgonja @humphreymgonja, ametembelea Shule ya Msingi Majengo iliyopo jijini Tanga kushuhudia jinsi mbinu hiyo inavyobadili uwezo wa watoto wa kusoma na kuandika. 🎥 @frankmavura - - #bbcswahili #elimu #watoto #tanga Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw