Tathmini mpya ya KCSE 2023 : Ujumlishaji mpya wa matokeo ya KCSE kuanza

  • | Citizen TV
    294 views

    Waziri wa Elimu Ezekiel Machogu ametangaza kuanzishwa kwa utekelezaji wa pendekezo la jopokazi kuhusu mabadiliko kwenye sekta ya elimu ambapo sasa matokeo ya mtihani wa KCSE yataanza kujumlishwa kwa njia tofauti. Akitangaza mikakati ya kuhakikisha mitihani ya kitaifa itakayoanza mwezi Novemba na kukamilika Disemba imekwenda sawa, Machogu amesema kuwa ujumlishaji wa matokeo ya KCSE utazingatia masomo mawili ya lazima ambayo ni Hisabati na lugha moja kati ya Kiingereza, Kiswahili na Lugha ya Ishara pamoja na masomo mengine matano.