Hospitali ya AGC Tenwek katika kaunti ya Bomet imeanzisha mpango wa kutumia mashine ya kusaidia wagonjwa wenye matatizo ya moyo kupitia teknolojia ya akiliunde maarufu AI ambayo inarahisisha uwezo wa wataalamu kugundua matatizo ya mgonjwa kwa kuchukua picha ya sehemu za mwili yenye matatizo kwa usaidizi wa teknolojia.
Madaktari wanasema teknplojia ya akiliunde ni njia mwafaka kinyume na njia za hapo awali ambapo teknolojia ya zamani ingelemaza uwezo wa kuwasaidia wagonjwa kwa haraka. Matumizi ya akiliunde imebadilisha sekta ya matibabu kwa haraka kwa kuimarisha usahihi wa uchunguzi, kuharakisha uvumbuzi wa tiba na dawa, utaratibu wa matibabu ya kibinafsi, na kuongezeka kwa ufanisi wa matokeo bora ya mgonjwa.