Skip to main content
Skip to main content

Tume ya ardhi yasema imesuluhisha kesi 1,066 nje ya korti

  • | Citizen TV
    192 views
    Duration: 1:39
    Tume ya ardhi nchini NLC imeendelea kukusanya taarifa kuhusu migogoro ya ardhi na dhuluma za kihistoria katika kaunti mbalimbali nchini. Kamishina wa Tume hiyo Tiyah Galgalo amesema jumla ya kesi 1,864 za migogoro ya ardhi zimewasilishwa na jamii kutoka maeneo tofauti, huku kesi 1,066 tayari zikiwa zimetatuliwa katika kipindi cha mwaka mmoja. Kwa sasa, Tume inaendelea kuzuru kaunti zote ili kusikiliza na kushughulikia masuala ya ardhi katika ngazi ya jamii.