Tume ya kulinda data yajitetea kwa kutangaza uamuzi wake wa kufuta leseni za Worldcoin

  • | K24 Video
    46 views

    Tume ya kulinda data imejitetea kwa kutangaza uamuzi wake wa kufuta leseni iliyotolewa kwa tools for humanity, mshirika wa worldcoin nchini Kenya, ikisema kuwa uamuzi huo ulitokana na kampuni hiyo kuendeleza ukusanyaji wa data nchini licha ya kupewa amri ya kusitisha. kamishna wa data, immaculate kasait, ameitaka pia kamati maalum ya bunge kuboresha sheria za ulinzi wa data kwani shughuli za Worldcoin nchini zimewatoa taka sikioni kuhusu udhaifu wa sheria iliyoko.