“Tunalinda Taifa au tunaharibu taswira ya Tanzania”

  • | BBC Swahili
    22,862 views
    #bbcswahili #siasa #utekaji #tanzania Mbunge wa Jimbo la Kawe nchini Tanzania, Askofu Josephat Gwajima, amekemea vikali vitendo vya utekaji vinavyoendelea nchini, akisema vinaiharibu taswira ya Tanzania kimataifa na kuvuruga mahusiano ya kidiplomasia. Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam hapo jana, Gwajima alisema amefanya utafiti binafsi na kubaini kuwa takribani watu 83 wametekwa katika miaka ya hivi karibuni. “Utekaji sio utamaduni wetu kama Watanzania, unatakiwa kukemewa. Ninatoka Kawe, ambapo tukio kama hili lilitokea kwa Ally Kibao. Alishushwa kutoka kwenye gari hadharani na baadaye mwili wake ukapatikana akiwa amefariki, Kama ni baba yako au mtoto wako aliyepitia hali hiyo, utajisikiaje?” @frankmavura - - #bbcswahili #siasa #utekaji #tanzania#kenya#uganda Subscribe kupata video motomoto kila siku kutoka BBC Idhaa ya Kiswahili https://www.youtube.com/channel/UCoerKKIKIMlDYaVFSTlsWGw